Meya wa Jiji la Lusaka nchini Zambia amewataka wauza majeneza kuondoka katika eneo la hospitali watafute sehemu nyingine ya kufanya biashara na kwamba wasipofanya hivyo kwa hiari watahamishwa kwa nguvu.
Miles Sampa amewapa wafanyabiashara hao hadi Machi 2020 wawe wametekeleza agizo hilo vinginevyo watahamishiwa katika maeneo ya makaburi.
Wagonjwa na ndugu zako wamelalamikia kitendo cha wafanyabiashara hao kufungua vibanda vya majeneza nje ya Chuo cha Utabibu (UTH) ambapo kuna mochwari. Ndugu hao wamedai kuwa wafanyabiashara hao wanawaogofya wagonjwa na hivyo kufanya uwezekano wao wa kupona kuwa mgumu.