Meli kubwa ya kifahari, Azamara Cruise imewasili katika Bandari ya Dar es Salaam ikiwa na watalii 600 kutoka Marekani, Japan, China, Taiwan na Uingereza.
Meli hiyo imetia nanga kwenye gati jipya la kisasa lililoboreshwa ambalo ni sehemu ya maboresho yanayoendelea bandarini hapo.