Mane aomba radhi kwa kushindwa kwenda Senegal

0
633

Mshambuliaji nyota wa timu ya Taifa ya Senegal na klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza ameomba radhi kwa kushindwa kwenda nchini mwake baada ya kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa mwaka 2019.

Mane mwenye umri wa miaka 27 alitunukiwa tuzo hiyo Januari 7 mwaka huu nchini Misri na alitarajia kwenda Senegal Januari 8 kwa ajili ya kusherehekea tuzo hiyo katika hafla ambayo Rais wa Senegal, Macky Sall alitarajia kuhudhuria.

Mane ambaye tayari ana magoli 11 hadi sasa amesema alishindwa kwenda nchini mwake kutoka na kuingilia kwa ratiba ya usafiri iliyokuwa nje ya uwezo wake, lakini ameahidi kuwa atakwenda kusherehekea na nduguze mapema atakapopata nafasi.

Mane alilazimika kurejea nchini Uingereza kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Januari 11, 2020 ambapo Liverpool itakabiliana na Tottenham Hotspur