Rais John Magufuli amerejea jijini Dar es salaam akitokea Chato Mkoani Geita baada ya kumaliza likizo.
Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mke wake Mama Janeth Magufuli kesho anatarajia kuanza ziara ya kikazi Visiwani Zanzibar.
Ijumaa Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ofisi ya usalama wa Taifa Zanzibar na Jumamosi atafungua hotel yenye hadhi ya nyota tano ya Varde Azam Luxury hotel and SPA iliyopo eneo la Mtoni.
Jumapili Rais Magufuli atashiriki maadhimisho ya miaka 56 ya mapinduzi ya Zanzibar.