Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi Mwita Waitara amehitimisha ziara yake mkoani Arusha kwa kukagua shule ambayo imejengwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa kushirikiana na wadau Mbalimbali.
Shule hiyo imekamilika katika kila idara ikiwa ni pamoja na maabara na chumba cha kompyuta.
Naibu waziri Waitara amempongeza mkuu huyo wa mkoa kwa ubunifu na amemtakia heri katika ujenzi wa maendeleo mkoani Arusha.