TADB yakopesha wakulima Njombe bilion 1.1

0
135

Zaidi ya shilingi Bilioni moja na Milioni Mia Moja zimekopeshwa na
Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB mkoani Njombe kwa ajili ya kuimarisha sekta ya kilimo na ufugaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini Japhet Justine amesema mikopo hiyo imewapa fursa wakulima kuanzisha viwanda
vya mazao yao hali inayopunguza changamoto ya uhaba wa masoko na hivyo
kunufaika na kazi zao.

Akiwa mkoani Njombe amefika katika kiwanda cha kusaga na kukoboa
mahindi cha mjasiriamali ili kujiridhisha matumizi sahihi ya mkopo
huo.