Raia wa Uingereza ahukumiwa jela Cyprus

0
186

Mahakama nchini Cyprus imemhukumu msichana mwenye umri wa miaka 19 raia wa uingereza kifungo cha miezi minne baada ya kudanganya kubakwa na genge la watu nchini humo.

Msichana huyo ameonekana mahakamani akilia kwa kujutia kitendo hicho alichokifanya.

Hukumu hiyo inakuja baada ya kesi hiyo kuhairishwa kwa muda wa miaka mitatu na kutakiwa pia kulipa faini ya paundi 125 .

Vikundi vya wanaharakati za wanawake wamejitokeza katika mahakama hiyo kupinga hukumu hiyo huku msichana huyo aliyekuwa akiishi nchini Cyprus amejipanga kurejea nchni uingereza.