NHIF yatoa Elimu ya vifurushi Kigoma

0
110

Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya – NHIF Anne Makinda amewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kuchangamkia Fursa ya Vifurushi vya Bima ya Afya vinavyotolewa na Mfuko huo ili kuepuka Gharama kubwa za matibabu pindi wanapougua.

Makinda ametoa rai hiyo katika hafla ya uzinduzi wa vifurushi vipya vya bima ya Afya vinavyotoa nafasi kwa kila mtanzania kupata huduma hiyo nakusisitiza kuwa serikali imeanzisha vifurushi hivyo ili kupunguza Gharama za matibabu kwa wananchi.