Waswahili wanasema “baada ya dhiki ni faraja,” usemi huu unadhihirika kwa wakazi wa kisiwa cha Bezi kata ya Kayenze wilayani Ilemela mkoani Mwanza, ambao sasa wataondokana na adha ya usafiri katika ziwa Victoria baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa kivuko cha MV Ilemela.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia kivuko hicho kilichogharimu shilingi billioni 2.7 kuingizwa majini kwaajili ya majaribio, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mhandisi Atashasta Nditiye amesema serikali imejipanga kuondoa changamato za usafiri katika ziwa Victoria.