Rais Dk. Shein afungua mradi wa maji na usafi wa mazingira

0
175

Wananchi zaidi ya laki mbili visiwani Zanzibar wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji na mazingira katika mkoa wa Mjini Magharibi.


Mradi huo uliojumuisha ujenzi wa matanki makubwa yatakayo sambaza maji katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ametoa rai kwa wananchi kutunza mradi huo pamoja na vyanzo vya maji vilivyopo katika maeneo yao kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.