Bunge la Venezuela lageuka kuwa uwanja wa mapambano

0
261

Nchini Venezuela bunge la Congress la nchi hiyo, pamoja na maeneo ya viwanja vya bunge yamegeuka kuwa uwanja wa mapambano baada ya kiongozi wa upinzani nchini humo Juan Guido, kuzuiwa na askari kuingia bungeni.

Ndani ya ukumbi wa bunge ngumi ziliendelea kati ya upande wa upinzani na wabunge wa chama tawala, huku nje ya bunge Guido akipambana na walinzi waliokuwa wakimzuia asiingie ndani, baada ya kujaribu kuruka uzio wa bunge.