Watu mashuhuri wajitokeza kusaidia janga la Moto Australia.

0
229

Baadhi ya wasanii wakubwa duniani wamejitoa kwa namna mbalimbali kusaidia janga la moto linaloendelea katika bara la Australia.

Moto huu unasemekana kuwa ni mkubwa mara tatu zaidi ya moto uliotokea Carlifornia mwaka 2018, na mara saba zaidi ya ule uliotokea Amazon mwaka jana.

Muigizaji Russell Crowe asitisha kuhudhuria tuzo za Golden Globes akibaki nyumbani kwake nchini Australia kuunga mkono jitihada za kusaidia maafa ya moto nchini humo. Picha: reuters

Bondia na muigizaji wa kimarekani Cody Rhodes amejitolea kuchangia asilimia 100 ya faida itakayopatikana baada ya kuuza mtindo mpya wa mashati yake kwa watoa huduma ya zimamoto huko New South Wales, Australia.

Muigizaji Russell Crowe naye ameamua kutohudhuria tuzo za Golden Globes ambapo ameshinda tuzo ya muigizaji bora ili kuweza kukaa na familia yake huko Australia.

Picha kuu: Picha ikionesha moto mkubwa ukiwa bado unawaka. Picha: vox.com