Mkazi wa jiji la Dar es Salaam Dkt.LOUIS SHIKA (Mia Tisa Itapendeza) moja ya watu wachache waliyojizolea umaarufu uliodumu kwa kipindi kifupi jijini Dar es salaam ,amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa matibabu.
Dkt. SHIKA ambaye katika siku za karibuni amekuwa akishinda na kulala katika maegesho ya magari katikati mwa jiji la Dar es salaam amelazwa katika hospitali hiyo kwa muda wa siku mbili sasa huku watu wake wakaribu wakisema bado hawajui anaugua ugonjwa gani.