Serikali imesema inakusudia kuvifuta vyama vya ushirika 3436 baada ya kubaini kuwa vyama hivyo havina uhai.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini DODOMA, Waziri wa Kilimo JAPHET HASUNGA amesema hatua hiyo imekuja baada ya kufanyika utafiti na kubaini vyama hivyo pia kukiuka masharti na taratibu za vyama vya ushirika
Aidha, Waziri HASUNGA ametangaza kuanza kutumika kwa aina 40 za mbegu bora mpya za kilimo ambazo tayari zimefanyiwa utafiti na kugundulika kuwa na sifa mbalimbali ikiwemo kutoa mavuno mengi pamoja uwezo wa kupambana na magonjwa ya mimea.