Rais Magufuli na Fursa za Utalii nchini Tanzania

0
223

Rais John Magufuli ametoa wito kwa watanzania kujenga utaratibu wa kufuga wanyamapori kupitia bustani za wanyama (Zoo) ili kuongeza idadi ya wanyama hao na kupanua fursa za utalii na ajira nchini.

Rais Magufuli pia amewapongeza baadhi ya watu walioanzisha bustani za wanyamapori akiwepo Luteni Generali Mstaafu Samwel Ndomba, Dar es salaam Zoo na Bahari zoo.

Aidha ameongeza kuwa ufugaji Wanyama unaruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Dkt. Magufuli amesema kuwa serikali yake imedhamiria kuongeza hifadhi za taifa ambapo katika kipindi cha miaka 4 imeongeza hifadhi za Taifa kutoka 16 hadi 22

Msanii Gabo akimlisha Twiga