Startimes wapongeza Juhudi za Dkt. Rioba watoa tuzo kwa TBCOnline

0
211

Shirika la Utangazaji Tanzania TBC kupitia kitengo cha maudhui mtandaoni TBC ONLINE imepokea Tuzo ya kuwa kinara na kutambulika katika kutoa habari kupitia mitandao ya kijamii na kukabidhiwa cheti na Startimes kwa kufanya vizuri katika muhula wa mwaka 2019

Akipokea cheti na zawadi Mkuu wa kitengo cha Online Hamisi Holela amesema katika mwaka 2020 TBC itaendelea kuboresha zaidi vipindi matukio na upatikanaji wa habari za ukweli na uhakika huku afisa habari wa Startimes Pendo Mango akipongeza juhudi za Mkurugenzi Mkuu kwa kuboresha na kuongeza vyanzo zaidi vya kuipata TBC