Wafugaji wa nyuki walia na waharibifu wa misitu

0
257

Uwepo wa shughuli mbalimbali katika maeneo ya hifadhi ya misitu imekuwa changamoto kwa baadhi ya wafugaji wa nyuki mkoani geita na kupelekea wafugaji kushindwa kufuga kwa ustadi kutokana na shughuli zinazoendelea katika hifadhi hizo.

Baadhi ya wafugaji wametoa malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu wakati akikabidhi mizinga mia mbili kwa wan avikundi kumi wa wilaya ya geita ambapo wamesema shughuli kama ufugaji,ukataji wa miti kwa ajili ya matimba pamoja na uchomaji wa mikaa huathiri zaidi zoezi zima la ufugaji wa nyuki.

Zaidi ya tani sita za asali na tani mbili za nta zimezalishwa katika misitu ya wilaya ya Geita kwa vikundi ishirini na sita kwa mwaka wa fedha 2018/2019 licha ya changamoto mbalimbali za kibinadamu zinazofanyika katika hifadhi za misitu wilayani humo.

Naibu Waziri Kanyasu amewahimiza wafugaji kuendelea kulinda rasilimali za misitu ambapo misitu hiyo itawasaidia kuleta mvua kipindi cha kilimo pamoja kulinda vyanzo vya maji na vile vile watumie kama kufuga nyuki ili kujiingizia kipato.

Mwandishi: Nazareth Ndekia