Mgombea wa kiti cha Urais nchini Guinea ya Bisau Umaro Cissoko Embalo kutoka chama cha Upinzani cha Movement for Democratic Alternation, ameibuka na ushindi baada ya kujipatia asilimia 54 ya kura.
Umaro Mokhtar Sissoko Embalo amemshinda Domingos Simoes Pereira wa chama tawala cha PAIGC na hivyo kumrithi Rais aliyemaliza muhula wake Jose Vaz.
Rais wa sasa wa nchi hiyo, Jose Mario Vaz alishindwa kuingia katika duru ya pili baada ya kutawala kwa muda wa miaka mitano.
Toka Vaz achukue hatamu za urais mwaka 2014, kumekuwa na mawaziri wakuu 7 huku mivutano ya kisiasa ikiathiria vibaya uchumi wa nchi hiyo pamoja na rushwa.
Umaro Mokhtar Sissoko Embalo, Rais mteule wa Guinea-Bissau anakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa mivutano ya kisiasa iliyoigubika nchi hiyo pamoja na visa vya ufisadi.
