Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro, imetangaza Faru Vicky (49), kuwa ndio Faru mkubwa zaidi kuliko Faru wote kwa sasa Kufuatia kifo cha Faru Fausta (57), ambaye alikuwa Faru mwenye umri mkubwa zaidi Duniani.
Faru Vicky anakadiriwa kuwa na miaka 49 na Mamlaka hiyo inafikiria pia kumtoa porini na kumpeleka Faru Vicky kwenye banda ambalo Fausta alikuwa akiishi ili kumsaidia na yeye katika kipindi hiki cha uzee wake na kumuepusha kushambuliwa na Fisi kwakuwa uzee unafanya ashindwe kujiokoa.