Ole Sendeka atoa siku 15 kukamilishwa kwa hospitali ya wilaya ya Wanging’ombe

0
280

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amemtaka Mkuu wa Wilaya Wanging’ombe Ally Kasinge na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Edeth Lukoa kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ifikapo Januaru 15 mwaka ujao kama ilivyoelekezwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Seleman Jafo.

Ole Sendeka ametoa maagizo hayo baada ya kufika eneo la mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo ambayo imeelezwa kuchelewa kukamilika kwa wakati huku fedha zilizopangwa kutumika shilingi Bilioni Moja na Nusu zikiwa zimemalizika zote.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya hiyo Ally Kasinge amesema kati ya majengo matano ambayo hayakukamilika kwa wakati wakati wa ziara ya Waziri Jafo, majengo matatu tayari yamekamilika ikiwemo chumba cha mionzi na stoo.

Mwandishi Tatu Abdallah