Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amewataka wadau wa Utalii nchini kufanya matamasha ya kukuza na kuendeleza utalii na utamaduni wakati msimu wa utalii ili watalii wengi waweze kushiriki katika matamasha hayo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la utalii la Lamadi lililofanyika wilayani Busega mkoani Simiyu, Kanyasu ametaka kila Tamasha litakaloanzishwa lifuate ratiba ya utalii ya mwaka mzima ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Busega, Tano Mwera amesema Tamasha hilo litachagiza utalii wa ndani na kuwafanya Watalii wa ndani kuwa mabalozi wa vivutio vya utalii.