Waziri Hasunga aridhishwa na Maandalizi Tanganyika

0
213

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, ameridhishwa na maandalizi ya Kitalu
kikuu cha uzalishaji wa vizazi mama vya Mbegu za PAMBA, kilichopo eneo
la Kekesea wilayani Tanganyika.

Akizungumza mkoani Katavi, Hasunga amewataka watalamu wa bodi ya
Pamba  kukifuatilia kitalu hicho ili kuhakikisha  mbegu zinazozaliwa
zinakuwa na ubora unaohitajika.

Kitalu hicho awali kiliwekwa wilayani Meatu mkoani Simiyu ambapo kwa
sasa kimehamishiwa wilayani Tanganyika mkoani Katavi.

Awali Waziri Hasunga ametembelea kitalu cha miche zaidi ya laki sita
ya korosho ambayo imeoteshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika
kwa kushirikiana na Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Tuungane ambapo
miche hiyo itagawiwa bure kwa wakulima wilayani humo.