Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya matukio ya 170,000 ya ukiukaji wa haki za binadamu husan kwa watoto yameripotiwa katika kipindi cha miaka 9 kuanzia mwaka 2010-2019 na kwamba matukio ya aina hiyo yanazidi kuongezeka ulimwenguni
Katika ripoti yake ya Miaka kumi kuhusiana na matukio hayo Umoja wa Mataifa umesema mashambulio katika maeneo mbalimbali ikiwemo shule , hospitali na migogoro ya kivita imechangia kwa kiasi kikubwa mauaji ya watoto ambapo inakadiriwa kuwa kwa siku zaidi ya watoto 45 hufariki.
Shirika la umoja wa mataifa linashughulikia watoto UNICEF limeripoti katika mwaka 2018 zaidi ya watoto ishirini na nne elfu wamefanyiwa unyanyasaji na wengine wapo hatarini hususan katika nchi za Syria,Yemen na Afghanistan.