0
151

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala amesema serikali inakusudia kuukausha na kuutunza mwili wa faru Fausta kwenye jumba la makumbusho eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Faru Fausta amekufa akiwa na umri wa miaka 57 na inaaminika ndiye faru aliyekufa akiwa na umri mkubwa zaidi duniani. “Fausta ndiye faru aliyewahi kuishi kwa umri mrefu zaidi ya wote (kwa wale ambao rekodi zao zimetunzwa) kwa kawaida faru huishi kati ya miaka 37 na 43” amesema Waziri Kigwangala

Pia Waziri Kigwangala amesema Fausta ameishi porini kabisa kwa zaidi kidogo ya miaka 54, na alipopata upofu wa macho na uzee miaka mitatu iliyopita.

Fausta aliishi katika bonde la Ngorongoro kwa maisha yake yote na kwa bahati mbaya hakubahatika kuzaa. “Tunakusudia kumkausha na kuutunza mwili wake kwenye jumba la makumbusho pale pale eneo la hifadhi ya Ngorongoro, aidha ninawapongeza sana wahifadhi wetu wa Ngorongoro kwa kazi nzuri ya kumtunza faru Fausta, faru wengine wengi waliopo eneo hili na Hifadhi yote kwa ujumla” amalizia Waziri Kigwangala