Watu Sita wafariki kwenye ajali Dodoma

0
165

Watu Sita wamefariki dunia na wengine kumi na wawili kujeruhiwa
katika ajali ya gari iliyohusisha daladala na lori aina ya fuso usiku
wa kuamkia leo Jijini Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Giles Muroto amethibitisha kutokea
kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa lori
kukwepa shimo la barabarani.