Waziri wa kilimo Japhet Hasunga Amesema kumekuwa na matokeo chanya ya uzalishaji wa mazao katika maeneo ambayo serikali imewekeza miundombinu ya skimu za umwagiliaji nchini.
Hasunga ameyasema, katika skimu za umwagiliaji uzalishaji wa mazao umeongekeza na kufikia tani 8 kwa hekta ukilinganisha na kiwango cha uzalishaji wa mazao cha Dunia ambacho hekta moja inazalisha tani 5. 5.
Amezitaja skimu za umwagiliaji zilizofikia tani 8 kwa hekta ni skimu ya Umwagiliaji ya Mbarali estate, kapunga rice project na Madibila zilizoko mkoani Mbeya pamoja na skimu zote za mkoa wa Morogoro ikiwemo skimu ya Dakawa.
Waziri wa Kilimo ameanza ziara ya siku tatu mkoani Katavi akikagua maendeleo ya sekta ya kilimo mkoani humo.