Watu zaidi ya 60 wakiwemo Raia 4 wa Uturuki wamepoteza maisha kufuatia mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali ya Somalia, idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko wa bomu lililotegeshwa kwenye gari imefikia zaidi ya watu 60
Hata hivyo idadi kamili ya waliopoteza maisha bado haijafahamika na taarifa zinaeleza kuwa idadi ya majeruhi na walio katika hali mbaya ni wengi hivyo Kuna uwezekano wa idadi ya waopoteza maisha katika shambulizi hilo kuongezeka.