Baadhi ya wananchi wanaopata huduma za afya katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es salaam wamelalamikia kutozwa fedha kwa baadhi ya huduma ambazo ni za bure
Wakitoa malalamiko yao kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, wananchi hao wamesema kutokuwa na uelewa wa taratibu za huduma katika hospitali hiyo kumesababisha wao kutozwa fedha zaidi kinyume na utaratibu uliowekwa na Serikali.