Soko la nane linatarajiwa kuzinduliwa Mkoani Geita katika wilaya ya Chato ambapo masoko hayo kwa ujumla yamekuwa chachu ya uuzwaji wa dhahabu ambapo wanunuaji na wauzaji wa madini hayo wamekuwa na imani na masoko hayo kutokana na kuwa na vifaa vya kisasa na usalama wa soko ambapo tangu kuzinduliwa kwa Masoko Mkoani Geita tani 3 za madini ya dhahabu zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 282.2 zimeshauzwa katika Soko kuu la Madini.
Tani 3 zilizouzwa katika Soko la Madini Jumla ya Kilo 766 zimetoka kwa wafanyabiashara wadogo (BROKERS) kutoka katika masoko madogo yaliyopo Mkoani Geita.
Hadi sasa wilaya ya Geita kuna masoko madogo ya KATORO , NYARUGUSU , LWAMGASA , NYAKAGWE, wilaya ya BUKOMBE, wilaya ya Mbogwe na Soko Kuu la Dhahabu Geita Mjini na leo ni Soko la wilaya ya Chato linalotarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Madini DOTO BITEKO.
Mwandishi Nazareth Ndekia,Geita