Ndege aina ya Fokker 100 ya Shirika la Bek iliyokuwa imebeba watu 100 imeanguka nchini Kazakhstan muda mfupi baada ya kupaa kutoka katika uwanja wa ndenge wa Almaty.
Maofisa wa uwanja wa ndege wa Almaty Wanasema ndege hiyo imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Almaty siku ya Ijumaa alfajiri.
Wahuduma wa maswala ya dharura wameelekea katika eneo hilo ambapo watu saba tayari wamethibitishwa kufariki lakini haijulikani iwapo kuna manusura wowote.
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea katika mji mkuu wa Kazakhstan wa Nur-sultan kutoka mji mkubwa wa Almaty.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Uwanja wa ndege wa Almaty zimeeleza kuwa ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 95 na wafanyakazi watano.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa moja na dakika 22 , kabla ya kugonga kizuizi kimoja na kuangukia nyumba ya ghorofa mbili.