WANANCHI wa vijiji vitatu vya kata za Kambikatoto na Mafyeko Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, wameridhia kutoa eneo la misitu lenye ukubwa wa hekta zaidi ya laki moja ili liwe hifadhi ya misitu, ambalo litahifadhiwa na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania TFS , ili kuthibiti uharibifu wa mazingira
Wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS Imeomba eneo hilo ili kutunza usholoba wa wanyama wanaotoka hifadhi ya Ruaha kwenda hifadhi ya Katavi na pori la akiba la Piti.