Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya TANZANIA PRISONS dhidi ya YANGA uliokuwa uchezwe kesho umesogezwa mbele hadi tarehe itakayopangwa tena
Mchezo huo uliokuwa uchezwe kwenye uwanja wa kumbukumbu ya SOKOINE jijini MBEYA umeahirishwa baada ya sehemu ya kuchezea (PITCH) kuharibika baada ya uwanja wa SOKOINE kutumika kwenye tamasha la
muziki lililofanyika usiku wa kuamkia leo
Katika hatua nyingine, Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeufungia kwa muda uwanja wa Kumbukumbu ya CCM SOKOINE kutokana na kuharibika kwa eneo la kuchezea
Taarifa iliyotolewa na bodi ya ligi (TPLB) imesema michezo iliyopangwa kuchezwa uwanjani hapo ukiwemo wa TZ PRISONS na YANGA imetakiwa kutafutiwa viwanja vingine
Taarifa hiyo pia imevielekeza vilabu vyote vinavyotumia uwanja huo, kuanzia vilabu vya ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili kutafuta viwanja mbadala.