AFC Bournemouth inaikaribisha Arsenal ikiwa chini ya kocha wake mpya nahodha wa zamani wa timu hiyo Mikel Arteta, Arteta atataka kudhihirisha kwamba kibarua alichopewa anakiweza na anauwezo wa kuvaa viatu vya kocha wake wa zamani ARSENE WENGER,kwani kocha aliyefutwa kazi UNAI Emery alishindwa kuirejesha ARSENAL katika makali yake.
Aston Villa inaikaribisha Norwich City,Chelsea inavaana na Southampton, FRANK LAPARD anataka kudhihirisha uwezo wake baada ya kuifunga SPURS chini ya MOURINHO ikiwa ni baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo.
CRYSTAL PALACE itakuwa mwenyeji wa WEST HAM UNITED, EVERTON chini ya kocha mpya CARLO ANCELOTTI inataka kurejesha makali yake inaikaribisha GODSON PARK BURNLEY.
Sheffield United inayonyemelea kucheza ligi ya mabingwa ULAYA mwakani itakuwa nyumbani kuwakaribisha wababe wa MANCHESTER UNITED, Watford.
Manchester United inaikaribisha Newcastle United,huu ni mchezo wa makocha wawili wachezaji wa zamani wa MANCHETER UNITED, STEVE BRUCE wa Newcastle United dhidi ya OLE GUNNAR SOLSKJAER ambaye anahaha kuhakikisha kikosi chake kinarejea katika ushindani baada ya kupoteza mchezo uliopita walipofungwa mabao MAWILI kwa BILA na Watford huku Newcastle United ikiibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya CRYSTAL PALACE.
LEICESTER CITY ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani inaikaribisha LIVERPOOL, kocha wa Leicester City BRENDON ROGERS baada ya kushindwa kuifunga MANCHESTER CITY, je ataongoza kikosi chake kuwafunga waajiri wake wa zamani LIVERPOOL wanaosaka taji lao 19 la EPL