Liverpool yatwaa Ndoo ya Klabu bingwa Dunia

0
467

Mabingwa wa Ulaya Liverpool wameweka rekodi nyengine baada ya kutwaa Ubingwa wa Klabu Bingwa Duniani baada ya kupata ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Flamengo

Mshambuliaji wa Liverpool Roberto Firmino alifunga bao pekee la ushindi dhidi ya Flamengo kwenye mchezo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa kimataifa wa Khalifa Mjini Doha, Qatar

Firmino alifunga bao hilo ndani ya dakika za nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika bila timu hizo kupata bao kwenye fainali hiyo ya klabu bingwa Dunia

Ushindi huo unaifanya Liverpool ikiongozwa na Meneja Jurgen Klopp kutwaa taji hilo la dunia kwa mara ya kwanza jambo linalowafanya wachezaji na mashabiki kuwa na furaha huku wakiweka rekodi yakubeba mataji matatu wakiwa na kombe la klabu bingwa na Super cup