Walioshiriki maandamano India watiwa mbaroni

0
501

Polisi nchini India wamewatia mbaroni zaidi ya watu Mia Moja waliokuwa wakishiriki katika maandamano ya kupinga muswada wa uhamiaji uliopitishwa na Mabunge yote mawili ya nchi hiyo, Muswada ambao wanauona kuwa ni wa kibaguzi.

Hasira za Waandamanaji zimeongezeka baada ya mahakama nchini humo kutangaza kuwa imeahirisha suala la kusikiliza kesi ya madai kuhusiana na muswada huo hadi mwezi Januari mwaka 2020, na leo Waandamanaji hao  walipanga kufanya maandamano makubwa zaidi.

Mabunge yote mawili ya India yamepitisha Muswada wa kuwapatia hifadhi ya kisiasa nchini humo Wakimbizi ambao wamekuwa wakikabiliwa na mateso katika nchi wanazotoka,  huku ukiwabagua waumini wa dini ya Kiislam.