Serikali yahimiza Mazingira Rafiki kwa Wafanyakazi

0
222

Serikali imezitaka kampuni na taasisi kuhakikisha zinaweka mazingira rafiki kwa wafanyakazi ili kuongeza ufanisi na kukuza uchumi kupitia kazi wanazofanya.

Akizungumza katika hafla ya Tuzo za Mwajiri bora kwa mwaka 2019 Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Jenista Mhagama amesema imefika wakati kwa wafanyakazi kujitathmini na kuwajibika katika kazi wanazofanya

Tuzo hizo zinaandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania ATE ambapo katika tuzo hizo Kampuni ya TBL imeibuka mshindi wa jumla na kufuatiwa na Geita Gold Mine na washindi wa tatu ni Kampuni ya Puma Energy