Donald Trump amekuwa Rais wa tatu katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya matumizi mabaya ya madaraka, hatua inayompeleka moja kwa moja katika kesi dhidi yake itakayoamua ikiwa atabakia madarakani au la, uamuzi utakaotolewa na Baraza la ‘Senate’

Bunge la Wawakilishi (Congress) limepigia kura mashtaka mawili kwamba Rais Trump ametumia vibaya mamlaka yake na kwamba alizuia shughuli za Bunge hilo
