PSPTB watupia jicho weledi kwa watendaji sekta ya ugavi na ununuzi nchini

0
165

Bodi ya wataalam wa ununuzi na ugavi nchini (PSPTB) imewataka waajiri wote hapa nchini kuhakikisha wanatuma taarifa za utendaji kazi za watumishi wa fani ya ugavi na manunuzi kwenye bodi hiyo mara moja ili kuiwezesha kufanya tathmini ya uwezo na uhitaji wa wataalam katika taasisi husika.

Katika kutekeleza jukumu hili la kisheria mwezi Oktoba 2019 PSPTB iliandika barua kwa taasisi za umma 572 nchini na kuzitaka kuwasilishwa taarifa za watumishi wote wanaofanya kazi za ununuzi na ugavi katika taasisi zao.

Kwa mujibu wa PSPTB mpaka sasa jumla ya taasisi 460 kati ya 572 zilizoandikiwa barua hizo bado hazijapeleka taarifa husika na hivyo kuikwamisha bodi hiyo kutekeleza wajibu wake wa kisheria katika kupanga, kuelekeza na kuratibu mahitaji ya wataalam wa ununuzi na ugavi na kuishauri serikali mahitaji halisi ya wataalam hao kataka taasisi mbalimbali za umma.

Aidha PSPTB imetoa wito kwa wakuu wa taasisi na waajiri wote nchini ambao hawajawasilisha taarifa za watumishi wanaofanya kazi za ununuzi na ugavi kwenye tasisi wanazoziongoza kupeleka taarifa hizo kabla ya tarehe 31 Januari 2020.
.