Wakati Mataifa mbalimbali yakitafuta suluhisho la Wakimbizi katika Bara la Ulaya, baadhi ya Wakimbizi wanaofika katika nchi hizo wamejikuta wakiwa katika mazingira duni.
Wakimbizi wapatao 450 kutoka katika mataifa mbalimbali Barani Afrika, wanaishi katika shule ya msingi ya Squat katika mji wa Lion nchini Ufaransa baada ya kukosa kambi maalum ya kuwahifadhi nchini humo.
Wakimbizi hao wamesema kuwa shule hiyo ambayo imekuwa makazi yao ya muda haina hadhi ya kuhifadhi Wakimbizi, kwani Wanawake na Wanaume wanalazimika kulala katika eneo moja, hali kadhalika kwa wagonjwa na watu ambao hawaumwi.
