Rais Magufuli Aipongeza Mahakama

0
182

Rais Dkt. John Magufuli amesema Ujenzi wa Mahakama utasaidia kupunguza ucheleweshwaji wa uendeshaji wa mashauri hivyo ameipongeza Mahakama kwa kuamua kujenga Mahakama hiyo wilayani Chato mkoani Geita.

Pia naipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kujenga gereza katika wilaya hii.

Mahakama sio majengo pekee, tangu mwaka 2015 tumeteua Majaji wa Mahakama ya Rufaa 11, Majaji wa Mahakama Kuu 39 na tumeajiri Mahakimu 396, Serikali itaendelea kuajiri Watumishi wa Mahakama kadri itakavyowezekana.

Natoa rai kwa vyombo vyote vinavyohusika na kutoa haki kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha haki za Watanzania zinapatikana kwa wakati.