Waasi wameshambulia mji wa Beni na kuuwa watu 22

0
418

Waasi wa kundi la ADF wameshambulia tena mji wa  Beni  katika  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuuwa watu 22 katika  eneo la  Ndombi na Kamango.

Waasi hao wanaelezwa kuwashambulia wakaazi hao kwa risasi na kuwauawa  wakiwemo wanawake na watoto  huku wengine wakijeruhiwa hata hivyo jeshi la nchi hiyo liliingilia kati na kupambana na waasi hao.

Mwenyekiti wa mashirika ya kutetea haki za binaadamu Cepadho Omar Kavota amelalamikia  jesh la nchi hiyo kwa kushindwa  kuwatokgomeza  waasi wa ADF.

Zaidi ya watu 100 wameuwawa katika mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na kundi hilo tangu Novemba 5 mwaka huu wakati huohuo viongozi wakuu wa nchi za Sahel wanakutana nchini Niger kujadili na kupatia ufumbuzi  mashambulizi yanayoendelea   katika maeneo ya ukanda huo ambayo yamekuwa yakijitokeza mra kwa mara.