Uchaguzi nchini Israel unatarajiwa kufanyika Machi Mbili mwaka 2020, na utakua ni uchaguzi wa Tatu kufanyika katika kipindi cha mwaka mmoja.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya ule uliofanyika Septemba 17 mwaka huu ambapo Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu na mpinzani wake mkubwa Benny Gantz hawakuweza kuunda Serikali hadi kufikia hatua ya kuvunjwa kwa Bunge.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema kuwa, njia pekee ya kuondoa mkwamo wa kisiasa nchini Israel ilikuwa ni kwa Viongozi hao wawili kugawana mamlaka, lakini imeshindikana kutokana na mashtaka yanayomkabili Waziri Mkuu Netanyahu.