Abiy akabidhiwa tuzo ya Nobel

0
474

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed hii leo amepokea rasmi tuzo ya Amani ya Nobel mjini Oslo, ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kuutatua mzozo wa mpaka na nchi jirani ya  Eritrea.

Akielezea sababu za kuchaguliwa waziri mkuu huyo, mwenyekiti wa kamati ya Nobel Berit Reiss-Andersen amesema  Kamati ya Nobel ya Norway imeamua kumtunuku tuzo ya amani ya Nobel, waziri mkuu Abiy Ahmed Ali kwa juhudi zake za kutafuta amani na ushirikiano wa kimataifa na hasa kuupatia ufumbuzi mzozo huo wa mpakani pamoja na kanda yote ya kaskazini mashariki mwa afrika.

Abiy Ahmed mwenye umri wa miaka 43 ni  mshindi wa kumi wa Tuzo ya Amani ya Nobel barani Afrika ambapo

mshindi wa kwanza kutoka afrika alikuwa  Albert Luthuli alyepata tuzo hiyo mnamo mwaka  1960 kwa sera yake ya amani dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.