Rais Magufuli atoa msamaha kwa Wafungwa 5,533

0
279

Katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 57 ya Jamhuri, Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa Wafungwa 5,533 wanaotumikia vifungo vyao katika magereza mbalimbali nchini.

Akihutubia katika maadhimisho hayo mkoani Mwanza, Rais Magufuli amesema kuwa, ametoa msamaha huo kutokana na mamlaka aliyonayo kisheria.

Amesema kuwa miongoni mwa Wafungwa waliopatiwa msamaha ni wale wote wenye vifungo vya mwaka mmoja ambao wamekaa gerezani kuanzia siku moja na kuendelea na wale waliotumikia vifungo vya muda mrefu na kubakiza mwaka mmoja.

Rais Magufuli ametoa wito kwa Wafungwa wote waliopatiwa msamaha kwenda kuwa Raia wema na kuacha kutenda vitendo viovu.