Tanzania Kuimarisha Sekta ya Uchukuzi

0
393

Serikali ya Tanzania imeahidi kuendelea kuimarisha Miundombinu ya usafirishaji ili kuboresha sekta ya uchukuzi na maendeleo ya wananchi kwa kuendelea kufufua usafiri wa treni , kukarabati , kutengeneza na kununua meli mpya

Rais Magufuli akisikiliza taarifa ya Miradi

Hayo yameelezwa leo Jijini Mwanza na Rais Magufuli wakati wa kuweka jiwe la msingi kwaajili ya ujenzi wa Chelezo , utengenezaji wa meli mpya na ukarabati wa meli za Mv Butiama na MV Victoria

Aidha Rais Magufuli ametoa pongezi kwa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano kwa kazi kubwa wanayoifanya na kumuomba Spika wa Bunge Job Ndugai kuweka bajeti ya kununua meli mpya mwakani.

Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dr. Ayub Rioba akiwa na watendaji wa TBC