Rais Magufuli aweka jiwe la Msingi Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Daraja

0
362

Rais Dkt. John Magufuli amemtaka mkandarasi wa Daraja la Kigongo Busisi ambalo litakuwa na urefu wa M 3200 kufanya kazi kwa bidii ili kukamilisha mradi huo mapema zaid ili kuchochea maendeleo ya wakazi wa Kanda ya Ziwa na Watanzania kwa Ujumla

Akizungumza wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya daraja hilo ambalo litakuwa daraja refu zaidi Tanzania na Afrika Mashariki Rais Magufuli amesema daraja hilo litagharimu kiasi cha bilioni 699.2 fedha za Tanzania ikiwa ni kodi inayokusanywa na Serikali ya Tanzania na kusema kuwa Serikali haijaomba mkopo ili kufanikisha mradi huo