Ljungberg aonja kichapo kwa mara ya kwanza

0
811

Kocha wa muda wa timu ya Arsenal, – Freddie Ljungberg ameonja kichapo kwa mara ya kwanza baada ya timu yake ikiwa nyumbani katika uwanja wa Emirates kufungwa mabao Mawili kwa Moja na Brighton & Hove Albion.

Mabao ya Brighton yamepachikwa wavuni na Neal Maupay na Adam Wester, wakati bao la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Alexander.

Kwa matokeo hayo, Arsenal imeporomoka hadi nafasi ya Kumi katika msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa imebaki na alama zake 19, wakati Brighton ikishikilia nafasi ya 13 ikiwa imefikisha alama 18.

Katika matokeo mengine Newcastle United ikiwa ugenini imeitandika Sheffield United mabao mawili kwa bila na kujizogeza hadi katika nafsi ya 11 ikiwa imefikisha alama 18.

Ligi Kuu ya England inaendelea kutimua vumbi wikiendi hii kwa kuzikutanisha Everton  iliyemtimu kocha wake Marco Silva dhidi ya Chelsea , Bournemouth inaikaribisha Liverpool,  wakati Tottenham Hotspur itacheza na Burnley.