Wafanyakazi Ufaransa wagoma kufanya kazi

0
636

Wasafiri katika maeneo mbalimbali nchini Ufaransa wamejikuta wakiwa njiapanda baada ya nchi hiyo kushuhudia mgomo mkubwa wa kufanya kazi unaoendelea nchini nzima.

Wasafiri wamejikuta wakiwa wamekwama katika viwanja vya ndege, vituo vya usafiri wa Reli, Treni, Mabasi na usafiri mwingine, baada ya Wafanyakazi nchini humo kushiriki katika mgomo wa kupinga mazingira ya kufanyia kazi.

Wafanyakazi hao pia wanapinga kuhusu mafao ambayo Ufaransa imetenga kwa ajili ya Wastaafu, ambapo wamesema kuwa fedha iliyotengwa kwa ajili ya Wastaafu ni kidogo ikilinganishwa na muda wa  watu hao walioutumia kulitumikia Taifa lao.

Wafanyakazi hao hawana dalili ya kusitisha maandamano yao na wanasema wataendelea kuandamana hadi hapo Serikali ya Ufaransa itakapotambua umuhimu wa Wafanyakazi.