Watu Hamsini na Sita wamekufa na wengine kadhaa hawajulikani walipo, baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama nchini Mauritania.
Habari zinasema kuwa, boti hiyo ilikuwa ikifanya safari zake kati ya Mauritania na Gambia.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa, boti hiyo ilizama baharini baada ya kuishiwa mafuta na watu wengine 183 waliokuwa ndani ya boti hiyo walinusurika baada ya kufanikiwa kuogelea hadi Pwani.
Zoezi la kuwafuta watu wengine waliokuwa ndani ya boti hiyo ambao bado hawajulikani walipo linaendelea.