Mgogoro wa CUF na ACT Wazalendo wazidi kufukuta

0
264

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha Wananchi (CUF), -Mussa Haji Kombo  amemuomba Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kuingilia kati mgogoro uliopo kati ya chama hicho na Chama Cha ACT Wazalendo.

Kombo ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari, huku akidai kuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF Seif Sharif  Hamad amekumbatia mali za chama hicho na amewatishia CUF wasijaribu kushusha bendera katika matawi ya ACT huko pemba ambazo awali zilikuwa ofisi za CUF.

Machi 19 mwaka huu,  aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF Seif  Sharif  Hamad   alihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT Wazalendo.